Jinsi ya kusajili Mfuko wa Hifadhi ya Jamii

MASHARTI:

Andika barua ya maombi na tafadhali ambatisha nakala za vitu vifuatavyo

 1. Mamlaka au Sheria inayoanzisha mfuko mf. Sheria ya Bunge
 2. Hati ya dhamana
 3. Ripoti ya ukaguzi wa mahesabu ya hivi karibuni
 4. Cheti cha tathimini ya mfuko kuthibitisha muundo, na uwezo wa kifedha wa mfuko
 5. Upembuzi yakinifu wa mfuko unaopendekezwa.
 6. Nakala zilizothibitishwa za:   (a) Cheti cha uandikishaji cha MWAJIRI au; (b)Cheti cha usajili wa jina la Biashara la MWAJIRI.

Jinsi ya kusajili Mfukowa Hifadhi ya Jamii mahali pa kazi

MASHARTI:

 Andika barua ya maombi na tafadhali ambatisha nakala za vitu vifuatavyo:

 1.  Mamlaka au Sheria inayoanzisha mfuko mf. Sharia ya Bunge Sababu ya Uanzishaji mf.Sheria ya Bunge
 2. Taarifa ya tathimini ya mfuko kuthibitisha muundo,na uwezo wa kifedha wamfuko.
 3. Jedwali la viwango vya michango itakayolipwa na kila mwanachama.

Jinsi ya kumsajili Mtunzaji

MASHARTI

Andika barua ya maombi na tafadhali ambatisha nakala zilizothibitishwa za vitu vifuatavyo:

 1.  Ripoti ya ukaguzi wa mahesabu ya hivi karibuni
 2. Cheti cha uandikishaji
 3. Cheti cha Usajiliwa CMA (iwapo umesajiliwa na Mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana Tanzania);
 4. Hatiza Makubaliano (MOU)

Jinsi ya kusajili Meneja Uwekezaji

MASHARTI

Andika barua ya maombi na tafadhali ambatisha nakala zilizothibitishwa za vitu vifuatavyo

 1. Nakala ya Cheti cha Biashara
 2. Leseni ya Biashara
 3. Taarifa ya mwaka

Maombi yote yatumwe kwa:

Mkurugenzi Mkuu,

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Jamii,

 Barabara ya New Bagamoyo, JENGO LA ALFA Kitalu Na. 25.

S.L.P 31846 Dar es Salaam, Tanzania. Simu:  (+255) 22 276 1683-4,  Faksi:  (+255) 22 276 1681, Barua pepe:   Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Go to top