Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii iliundwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135 (Toleo la 2015) kwa lengo la kusimamia na kudhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa manufaa ya Wanachama na Taifa kwa ujumla. Mamlaka ilianza kazi rasmi mwishoni mwa Mwaka 2010.

 

Mamlaka ina jukumu la msingi la kuhakikisha kwamba Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inakuwa endelevu, inaendeshwa kwa kufuata kanuni, taratibu na kisheria, wanachama wanapata taarifa za Mifuko/michango yao, na mafao yaliyobora.

Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA ) kulifanywa ili kuhakikisha kwamba Sekta ya Hifadhi ya Jamii inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni,

Go to top