Kazi za Mamlaka zimeainishwa bayana chini ya Kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135 (Toleo la 2015) Kazi hizo ni pamoja na :-

 1. Kusajili Mifuko, Watunzaji na Meneja wa uwekezaji katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
 2. Kudhibiti/kurekebisha na kusimamia utendaji wa Mifuko, Watunzaji na Meneja wa uwekezaji
 3. Kutoa miongozo ya utendaji sahihi na yenye ubora katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
 4. Kutetea na kulinda maslahi ya wanachama
 5. Kusaji na Kusimamia Watawala/Administrators katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii
 6. Kumshauri Waziri juu ya Sera kuhusiana na Sekta ya Hifadhi ya Jamii
 7. Kupanga na kutangaza rasmi miongozo itakayotumika kwa Mifuko, Watunzaji na Wawekezaji
 8. Kusimamia na kupitia upya utendaji wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
 9. Kuanzisha mafunzo, kushauri,kuratibu na kutekeleza mabadiliko ya sheria katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
 10. Kumteua mtu atakayesimamia Mifuko pale inapobidi
 11. Kurahisisha upanuzi wa wigo wa Hifadhi ya Jamii kuwafikia wale ambao bado hawajafikiwa ikiwa ni pamoja na makundi/sekta zisizo rasmi.
 12. Kuendesha mipango ya elimu na uhamasishaji kwa umma juu ya masuala ya Hifadhi ya Jamii.
Go to top