• MMM
 • 1. PSSSF ni nini?

  JIBU: PSSSF ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma iliyoundwa kwa sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ya Mwaka 2018. Dhumuni la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kukusanya michango na kutoa mafao ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma. Pamoja na mambo mengine yanayohusiana na Hifadhi ya Jamii, Sheria hii ndio inafuta zilizokuwa sheria ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Sheria ya Mfuko wa Kustaafu wa GEPF na Mfuko wa Pensheni wa PPF

 • 2. Nini sababu ya kuunganisha iliyokuwa Mifuko ya Pensheni ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF

  JIBU: Lengo la kuunganisha kwa hii Mifuko ni pamoja na:

  • Kuwatenganisha watumishi wa umma na watumishi katika sekta binafsi kwa kuzingatia tofauti za ajira zao.
   • Kustaafishwa kwa manufaa ya umma
   • Tofauti ya viwango vya uchangiaji
   • Kuondoa malalamiko ya kuchangia marambili kwa watumishi wa umma (bima ya afya na SHIB)
  • Kupunguza gharama za uendeshaji zinazotokana na ushindani
  • Mifuko yote inatoa mafao yanayofanana
 • 3. Je Mfuko wa PSSSF inatoa Huduma kwa wafanyakazi wa aina gani?

  JIBU: Mfuko wa PSSSF inahudumia makundi yafuatayo ya Watumishi:

  • Watumishi wote wa Serikali Kuu
  • Watumishi wote wa Serikali za Mitaa
  • Watumishi wote Taasisi za Umma
  • Watumishi wote wa Magereza, Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji
  • Wanachama wa sasa wa PSPF, LAPF, GEPF na PPF
 • 4. Ni nini jukumu la Bodi ya Wadhamini?

  JIBU: Majukumu ya BODI ya Wadhamini wa Mfuko wa PSSSF ni:

  • Wanawajibika kusimamia Mfuko
  • Kuidhisha na kusimamia uwekezaji
  • Kuidhinisha malipo yoyote kutoka kwenye Mfuko
  • Wajumbe watawajibika personally kwa hasara yoyote katika Mfuko
 • 5. Mfumo wa Uchangiaji katika Mfuko wa PSSSF ukoje?

  JIBU: Mfumo wa Uchangiaji katika Mfuko wa PSSSF upo katika kiwango cha uchangiaji cha  20/% (15% Mwajiri x 5 Mfanyakazi)

 • 6. Vigezo gani vimewekwa ili mtu apate mafao?

  JIBU: Kifungu cha 26 cha Sheria imeainisha vigezo vya kupata mafao kama ifuatavyo;

  • Kufikisha umri wa kustaafu (Miaka 55 kwa hiari au 60 kwa lazima)
  • Sababu za ugonjwa
  • Kuachishwa kazi kwa maslahi ya umma
  • Kukoma kwa ajira kwa sababu ya teuzi za kikatiba
 • 7. Mafao yapi yatatolewa na Mfuko wa PSSSF?

  JIBU: Kifungu cha 29 cha Sheria imeainisha Mafao yafuatayo;

  • Mafao ya pensheni;
  • Mafao ya warithi;
  • Mafao ya ulemavu;
  • Mafao ya ugonjwa;
  • Mafao ya uzazi;
  • Mafao ya ukosefu wa ajira;
  • Mafao ya kifo; na
  • Kafao ya mazishi.

  Mafao yote yatagharimiwa na kiwango kile kile cha asilimia 20.

 • 8. Je ni mafao yapi yameongezeka kutoka kwenye idadi ya mafao ya zamani?

  JIBU: Mafao mapya mawili ambayo yameongezeka ni fao la ukosefu wa ajira na fao la ugonjwa.

 • 9. Je mwanachama anawezakutumia mafao yake kupata mikopo ya nyumba kama sehemu ya maandalizi ya kustaafu?

  JIBU: Ndio, Kifungu cha 42 cha Sheria ya Mfuko inaruhusu mwanachama kutumia sehemu ya Mafao yake kupata mkopo wa nyumba

 • 10. SSRA ni nini?

  Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii iliundwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135 (Toleo la 2015) kwa lengo la kusimamia na kudhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa manufaa ya Wanachama na Taifa kwa ujumla. Mamlaka ilianza kazi rasmi mwishoni mwa Mwaka 2010.

   

  Mamlaka ina jukumu la msingi la kuhakikisha kwamba Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inakuwa endelevu, inaendeshwa kwa kufuata kanuni, taratibu na kisheria, wanachama wanapata taarifa za Mifuko/michango yao, na mafao yaliyobora.

  Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA ) kulifanywa ili kuhakikisha kwamba Sekta ya Hifadhi ya Jamii inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni,

 • 11. Nini Wajibu Na Majukumu ya SSRA

  Wajibu na Majukumu ya Mamlaka zimeainishwa bayana chini ya Kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya Jamii Kazi hizo ni pamoja na :-

  i. Kusajili Mifuko, watunzaji na Meneja wa uwekezaji katika sekta ya Hifadhi ya Jamii.
  ii. Kudhibiti/kurekebisha na kusimamia utendaji wa Mifuko, watunzaji na Meneja wa uwekezaji
  iii. Kuweka mazingira yatakayopanua uwigo wa hifadhi ya Jamii na kuongeza wanachama hasa kwenye sekta isiyo rasmi
  iv. Kutoa miongozo ya utendaji sahihi na yenye ubora katika sekta ya Hifadhi ya Jamii.
  v. Kutetea na kulinda maslahi ya wanachama
  vi. Kuweka mazingira mazuri na yanayofaa kukuza na kuendeleza Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
  vii. Kumshauri Waziri juu ya Sera na Masuala ya uendeshaji kuhusiana na Sekta ya Hifadhi ya Jamii
  viii. Kupanga na kutangaza rasmi miongozo itakayotumika kwa mifuko, watunzaji na wawekezaji
  ix. Kusimamia na kupitia upya utendaji wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
  x. Kuanzisha mafunzo, kushauri,kuratibu na kutekeleza mabadiliko ya sheria katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
  xi. Kumteua mtu atakayesimamia Mifuko pale inapobidi
  xii. Kurahisisha upanuzi wa wigo wa hifadhi ya jamii kuwafikia wale ambao bado hawajafikiwa ikiwa ni pamoja na makundi/sekta zisizo rasmi.
  xiii. Kuendesha mipango ya elimu na uhamasishaji kwa umma juu ya masuala ya hifadhi ya jamii.

 • 12. Mfumo wa Hifadhi ya Jamii ukoke nchini Tanzania?

  Nchini Tanzania mfumo wa Hifadhi ya Jamii umegawanyika katika nguzo tatu (3), kama ifuatavyo;

  i. Nguzo ya kwanza- nguzo hii inahusisha Hifadhiya Jamii kwa mfumo wa huduma za kijamii zinazogharamiwa na kodi ya Serikali, mashirika ya wahisani wa ndani na nje na taasisi za kijamii
  ii. Nguzo ya pili- katika nguzo hii, Hifadhi ya Jamii inahusisha uchangiaji walazima wa wenye kipato na waliona ajiriwa na ndio nguzo ambayo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inahusika. Uchangiaji katika mifuko hiyo ugharamiwa na Waajiri pamoja na Wafanyakazi.
  iii. Nguzo ya tatu- Hifadhi ya Jamii katika nguzo hii hutolewa kwa mfumo uchangiaji wa hiari ambao unawalenga zaidi watu wenye kipato cha ziada na huchangia kama ziada baada ya kutekeleza majukumu ya kisheria kwenye nguzo ya pili.

 • 13. Je Kuna mifuko mingapi ya Hifadhi ya Jamii Tanzania?

  Kuna mifuko sita ya Hifadhi ya jamii Tanzania bara, ambayo ni:
  i. Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF )
  ii. Mfuko wa Pensheni wa LAPF
  iii. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
  iv. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
  v. Mfuko wa Pensheni wa PPF (PPF)
  vi. Mfuko wa Pensheni wa PSPF (PSPF)
  Mifuko yote hii inasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)

 • 14. Ni mafao yapi yatolewayo na mifuko ya hifadhi ya jamii?

  Kuna aina mbili za mafao yatolewayo na mifuko ya hifadhi za jamii Tanzania, yapo mafao ya muda mfupi na yale ya muda mrefu.

  a) Mafao ya Muda mrefu

  i. Mafao ya uzeeni
  ii. Mafao ya Ulemavu
  iii. Mafao ya Urithi

  b) Mafao ya Muda Mfupi

  i. Huduma za Afya
  ii. Kuumia Kazini
  iii. Uzazi
  iv. Kifo
  v. Elimu

 • 15. Kwanini mafao ya wanachama yamepunguzwa?

  Mafao hayajapunguzwa bali yameongezwa kwa asilimia 37.5 ambayo pia yalizingatia thamani ya ulipwaji wa pensheni unaendana na gharama za maisha (Indexation). Maboresho hayo yametojana na tathmini za kitaalamu pamoja na maoni ya wadau

 • 16. Mafao mapya yana anza lini?

  Kanuni za Mafao mapya zimeshaanza kutumika rasmu tarehe 01/07/2014, kanuni hizi zimeanza kutumika kwa wanachama wanaostaafu Mfuko a NSSF, PPF na GEPF, hata hivyo kanuni hizi haziwagusi wanachama waliokuwapo PSPF na LAPF kabla ya tarehe 01/07/2014.

 • 17. Kuna umuhimu gani wa kuwa na Mifuko mingi kwa mfano yamelinganishwa kwa Mifuko yote?

  Mwanzoni Mifuko ilianzishwa kisekta. Hata hivyo baada ya kuwianisha mafao, SSRA imepata watathmini Shirika la Kazi duniani (ILO) kufanya tathmini yenye kuangalia namna bora ya kuunganisha Mifuko ikiwa ni pamoja na gharama zitakazojitokeza katika zoezi hilo.

 • 18. Kwanini Mafao ya Kifo yanacheleweshwa sana?

  Mafao ya kifo ucheleweshwa kutokana na uhitaji wa hatua nyingi za uhakiki, SSRA kwa kushirikiana na ILO na Mifuko husika wanalifanyia kazi swala hilo

 • 19. Mafao mapya yana anza lini?

  Kanuni za Mafao mapya zimeshaanza kutumika rasmu tarehe 01/07/2014, kanuni hizi zimeanza kutumika kwa wanachama wanaostaafu Mfuko a NSSF, PPF na GEPF, hata hivyo kanuni hizi haziwagusi wanachama waliokuwapo PSPF na LAPF kabla ya tarehe 01/07/2014.

 • 20. Kuna umuhimu gani wa kuwa na Mifuko mingi kwa mfano yamelinganishwa kwa Mifuko yote?

  Mwanzoni Mifuko ilianzishwa kisekta. Hata hivyo baada ya kuwianisha mafao, SSRA imepata watathmini Shirika la Kazi duniani (ILO) kufanya tathmini yenye kuangalia namna bora ya kuunganisha Mifuko ikiwa ni pamoja na gharama zitakazojitokeza katika zoezi hilo.

 • 21. Kwanini Mafao ya Kifo yanacheleweshwa sana?

  Mafao ya kifo ucheleweshwa kutokana na uhitaji wa hatua nyingi za uhakiki, SSRA kwa kushirikiana na ILO na Mifuko husika wanalifanyia kazi swala hilo

 • 22. Je itachukua muda gani mifuko ya PSPF na LAPF kulipa kwa kutumia kikokotoo kipya?

  Inakadiriwa kwamba itachukua kati ya miaka 25-35 kwa Mifuko hii kulipa kwa kutumia kikokotoo kipya kwa vile kinaanza na wanachama wapya waliojiunga Julai 1,2014.

 • 23. Jinsi gani Mifuko ya Pensheni uhusisha Wanachama katika kufanya maamuzi

  Mifuko ya Pensheni uhusisha wanachama na wadau wengine katika kufanya maamuzi kupitia kwa muundo wa Bodi ya Wadhamini linaloshirikisha wadau wa sekta ya hifadhi ya ya jamii katika utungaji wa sera na kufanya maamuzi mengine makubwa kama inavyoelekezwa katika muongozo uendeshaji wa bodi ya wadhamini uliotolewa na mamlaka ya hifadhi ya jamii SSRA
  Mkutano Mkuu wa Mwaka ni njia nyingine ya ushiriki muhimu wa wanachama kuhusika katika uendeshaji wa mifuko

 • 24. Kwa nini Pensheni si kulipa gawio?

  Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya lazima Tanzania ni Define Benefits yaani ni mifuko ya pensheni inayofuata misingi ya kibima Mwanachama huahidiwa mafao mbalimbali pamoja na pensheni. Hapa risk ya kuishi muda mrefu pamoja na risk ya uwekezaji hubebwa na mifuko

 • 25. Umri wa kustaafu nchini Tanzania ni upi?

  Kisheria umiri wa kustaafu kwa hiari nchini Tanzania ni miaka 55, na miaka 60 kwa lazima, japokuwa kuna baadhi ya sekta zina umri tofauti wa kustaafu.

Go to top